Mwenyekiti wa shirikisho la kandanda ulimwenguni, FIFA, Sepp
Blatter, amesisitiza ilikuwa kosa kuchagua Quatar kuwa mwenyeji wa kombe la
dunia la mwaka wa 2022.
Alijibu kwa kukiri na kuongeza kuwa kila mtu hukosea maishani. Alipinga madai kwamba taifa hilo lilikuwa limelipia michezo hiyo.
Aliongeza kuwa kamati inayojumuisha maafisa wa FIFA walikuwa wamedhibitisha uwezekano wa taifa hilo kuwa mwenyeji ijapokuwa walikuwa wamepokea taarifa kuhusu vipimo vya juu vya joto.
Alisema kwamba michezo hiyo badala yake inaweza kusogezwa hadi miezi ya mwisho wa mwaka, wakati vipimo vya joto vitakuwa vimepungua.
No comments:
Post a Comment