BAADA ya kupewa nafasi ya kushiriki tuzo ya Televisheni ya Marekani
(BET), akiwa ni msanii pekee ambaye anaiwakilisha Afrika Mashariki, Naseb Abdul
‘Diamond Platinum’ amesema anawashukuru Watanzania kwa kumtambua kama ni msanii
bora.
Diamond amepata nafasi hiyo baada ya kupata tuzo saba za
Kilimanjaro Tanzania Music Awards (KTMA), pia ilipelekea kuwa msanii pekee wa
Tanzania ambaye atafanya ziara ya shoo ya MTV Base Afrika Music Award (MAMA)
ambayo inaanzia Dar es Salaam katika
ukumbi wa Club Bilicanas leo.
Akizungumza na Indaba Blog jijini Dar es Salaam jana,
Diamond alisema anatoa shukrani kwa Watanzania ambao wamezidi kung’arisha nyota
yake mpaka katika nchi za kimataifa.
“Nawashukuru sana Watanzania kwa kunikubali katika kazi zangu
ambazo kwasasa zimeanza kuvuka mipaka ya Tanzania na mpaka kuchaguliwa katika
tuzo hizo kubwa Duniani hivyo nahitaji sapoti sapoti yao zaidi ili niweze kupaa
katika mataifa mbalimbali,” alisema.
Alisema, anafikiri haishii kushiriki tu anauhakika atachukua
tuzo katika televisheni hiyo ambapo amewataka Watanzania kuendelea kumuombea.
Wasanii ambao wanachuana na Diamond katika tuzo hizo wakiwania
tuzo ya msanii bora wa Afrika ni, Davido na Tiwa Savage wa Nigeria, Mafikizolo
(Afrika Kusini), Sarkodie (Ghana) na Toofan (Togo).
No comments:
Post a Comment