Kutoka kushoto ni Katibu wa Katibu wa TAFF , Bishop Hiluka, Amil Shivji, Rais wa TAFF, Simon Mwakifwamba akimkabidhi tuzo hiyo na Mwenyekiti Suleiman Ling'ande.
SINEMA ya ‘Shoe shine’ inayotumia muda wa dakika 24 iliyofyatuliwa mwaka 2013 iliyotengenezwa na kuongozwa na Amil
Shivji imefanikiwa kupeperusha vema
bendera ya nchi na kupata tuzo katika tamasha la kimataifa la filamu
lililofanyika nchini Burundi (Festicab 2014) kati ya Juni 13 hadi 20 ambapo lilifikia kilele.
Sinema hiyo
ambayo ni fupi lakini iliyotimiza wajibu wake kwa kuzingatia maudhui na
kuweza kufikisha ujumbe kwa hadhira ndiyo filamu pekee iliyoshinda katia
ya sinema tatu zilizokuwa zikiwania tuzo hizo.
Katika
tamasha hilo ambalo lilishirikisha
sinema mbalimbali kutoka nchi za
Tanzania, Kenya,Uganda, Rwanda, Burundi, Senegal, Cameroon, Morocco, Misri,
Ufaransa, Benin, Madagascar na Burkina
Faso.
Nchi zingine
ni Afrika ya Kati, Afrika Kusini
,Tunisia, DR Congo, Gabon na Marekani
ambazo zilishindanishwa katika vipengele tofauti tofauti huku Tanzania ikiingiza
sinema zake tatu tu ambazo ni
‘Mdundiko’(2013),iliyoongozwa na Jackson
Kabirigi, ‘Anguko’ (2013),
iliyoongozwa na Edgar Ngelela na
‘Shoe shine’ Amil Shivji.
Akizungumza
na waandishi wa habari katika mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam leo asubuhi Rais wa
Shirikisho la Filamu nchini (TAFF), Simon Mwakifwamba alisema kuwa tuzo hiyo ya
filamu ya Shoe Shine ni darasa kwa wasanii wa hapa nchini kuweza kutunga filamu
fupi na zenye kufikisha ujumbe wakati.
“nachukua
fursa hii kuipongeza kumpongeza muandaaji wa Sinema ya Shoeshine kwa kufanikiwa kuipeperusha vema bendera ya
nchi huko Burundi kwani ametutangaza kimataifa inatia moyo wasanii wengine
waige mfano wake ni darasa la kutosha” alisema Mwakifwamba.
Tuzo
hii ya sinema fupi bora Afrika
Mashariki ilipokelewa na Katibu
wa TAFF Bishop Hiluka kwa niaba ya Shivji.
Pia sinema hii imeingia kwenye mchujo wa kuwania tuzo yz ‘Best Short Film’ kwenye kituo cha
Africa Magic Viewer’s Choice Awards 2014.
Aidha
imechaguliwa kuoneshwa katika matamasha
ya Kimataifa ya filamu ambayo ni Rotterdam, Luxor
African,Tamasha la 36 la Durban,Film Africa, Euro African,Tamasha la filamu la
44 la Tempere na tamasha la filamu la 33 la Verona African.
Mwakifwamba
alimalizia kwa kusema kuwa kwa kupitia
kazi yake hii, Shivji amepata pesa
kupitia mfuko maalum wa kuwawezesha watengeneza sinema fupi wa Afrika
‘Africa First Features grant’ , baada ya script yake kushinda kipengele cha 2013, kwa sasa yupo
mbioni kumalizia kazi yake mpya iitwayo ‘Samaki Mchangani’.