Tuesday, 1 July 2014

AMIL SHIVJI AIBUKA APATA TUZO YA FILAM FUPI BUJUMBURA BURUNDI


Kutoka kushoto ni Katibu wa Katibu wa TAFF , Bishop Hiluka, Amil Shivji, Rais wa TAFF, Simon Mwakifwamba akimkabidhi tuzo hiyo na Mwenyekiti Suleiman Ling'ande.
SINEMA ya ‘Shoe shine’  inayotumia muda wa dakika 24 iliyofyatuliwa mwaka 2013  iliyotengenezwa na kuongozwa na Amil Shivji  imefanikiwa kupeperusha vema bendera ya nchi na kupata tuzo katika tamasha la kimataifa  la filamu  lililofanyika nchini Burundi (Festicab 2014) kati ya Juni 13  hadi 20 ambapo lilifikia kilele.

Sinema hiyo ambayo ni fupi lakini iliyotimiza wajibu wake kwa kuzingatia maudhui  na  kuweza kufikisha ujumbe kwa hadhira ndiyo filamu pekee iliyoshinda katia ya sinema tatu zilizokuwa zikiwania tuzo hizo.

Katika tamasha hilo ambalo lilishirikisha  sinema mbalimbali kutoka  nchi za Tanzania, Kenya,Uganda, Rwanda, Burundi, Senegal, Cameroon, Morocco, Misri, Ufaransa, Benin, Madagascar na  Burkina Faso.

Nchi zingine ni  Afrika ya Kati, Afrika Kusini ,Tunisia, DR Congo, Gabon na  Marekani ambazo zilishindanishwa katika vipengele tofauti tofauti huku Tanzania  ikiingiza  sinema  zake tatu tu  ambazo ni  ‘Mdundiko’(2013),iliyoongozwa na Jackson  Kabirigi, ‘Anguko’ (2013),  iliyoongozwa na  Edgar Ngelela na ‘Shoe shine’ Amil Shivji.

Akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam  leo asubuhi  Rais wa Shirikisho la Filamu nchini (TAFF), Simon Mwakifwamba alisema kuwa tuzo hiyo ya filamu ya Shoe Shine ni darasa kwa wasanii wa hapa nchini kuweza kutunga filamu fupi na zenye kufikisha ujumbe wakati.

“nachukua fursa hii kuipongeza kumpongeza muandaaji wa Sinema ya Shoeshine  kwa kufanikiwa kuipeperusha vema bendera ya nchi huko Burundi kwani ametutangaza kimataifa inatia moyo wasanii wengine waige mfano wake ni darasa la kutosha” alisema Mwakifwamba.

Tuzo hii  ya sinema fupi  bora Afrika  Mashariki  ilipokelewa na Katibu wa TAFF Bishop Hiluka kwa niaba ya Shivji.

Pia  sinema hii imeingia  kwenye mchujo wa kuwania  tuzo yz ‘Best Short Film’ kwenye kituo cha Africa Magic Viewer’s Choice Awards 2014.

Aidha imechaguliwa  kuoneshwa katika matamasha ya  Kimataifa  ya filamu ambayo ni Rotterdam, Luxor African,Tamasha la 36 la Durban,Film Africa, Euro African,Tamasha la filamu la 44 la Tempere na tamasha la filamu la 33 la Verona African.

Mwakifwamba alimalizia kwa kusema kuwa  kwa kupitia kazi yake hii, Shivji amepata pesa  kupitia mfuko maalum wa kuwawezesha watengeneza sinema fupi wa Afrika ‘Africa First Features grant’ , baada ya script yake  kushinda kipengele cha 2013, kwa sasa yupo mbioni kumalizia kazi yake mpya iitwayo ‘Samaki Mchangani’.

No comments:

Post a Comment