Kocha wa Chelsea Jose Mourinho amesema kuwa Mshambulizi wa
galatasaray ya Uturuki Didier Drogba ni Mchelsea damu .
"Nikifaulu kumrejesha Uingereza jambo ambalo natumai litafanyika kwa haraka ,itakuwa kwa sababu ya uwezo wake mkubwa wa kuimarisha kikosi na timu kwa jumla''.
Drogba, alijiunga na Chelsea mwaka wa 2004 akitokea Marseille katika uhamisho ulioigharimu klabu hiyo pauni milioni £24.
Wakati huo aliiongoza Chelsea kutwaa mataji matatu ya ligi kuu ya Uingereza mataji 4 ya FA , mataji mawili madogo ya ligi mbali na ubingwa wa bara Ulaya .
No comments:
Post a Comment