
Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan ameagiza kufanywa oparesheni
kali zaidi ili kudhibiti alichokiita mauaji ya kiholela yanayofanywa na
magaidi.
Rais Jonathan pia ameahidi kufanya mashauriano na upatanishi na watu watakaoweka silaha chini na kukoma kujihusisha na ugaidi.
Rais Jonathan ameahidi kushughulikia swala la umasikini ambalo limechochea harakati kama za Boko Haram, lakini akasisitiza hilo litafanyika tu ikiwa ugaidi unaotendwa na Boko Haram utakapokomeshwa.

Rais Goodluck, ametoa fursa kwa Boko Haram ikiwa wanataka kufanya mazungumzo na serikali kama njia ya kusuluhisha matatizo yao.
Maelfu ya watu wameuawa katika miaka mitano ya harakati za kundi hilo.Mwaka huu pekee watu 2,000 wameuawa huku zaidi ya wengine 750,000 wakiachwa bila makao.
No comments:
Post a Comment