Polisi nchini Brazil wametumia gesi ya kutoa machozi
kuwatawanya waandamanaji katika mji mkuu Brasilia wanaopinga kuandaliwa kwa
kombe la dunia nchini humo.

Kikundi cha watu asilia wanaodai haki zao za kumiliki ardhi walijiunga na maandamano hayo.
Haya ni maandamano ya hivi karibuni nchini Brazil kupinga gharama iliyotumiwa kuandaa kombe hilo.
Maafisa wakuu wanasema kuwa karibu watu 1,500 walihudhuria maandamano hayo yaliyofanyika Jumanne.
Waandamanaji hao walijaribu kwenda katika uwanja wa kitaifa ambao utakuwa mwenyeji wa mechi kadhaa za kombe la dunia ingawa polisi waliwazuia.
Polisi mmoja alijeruhiwa kwa mshale uliorushwa na mmoja wa waandamanaji wakati wa makabiliano kati ya polisi na waandamanaji hao.
Waandamanaji hao walitatiza pakubwa msongamano wa magari mjini Brasilia kwa masaa kadhaa.
Mwaka jana takriban watu milioni moja walishiriki maandamano kote nchini humo kutaka huduma bora zaidi za umma na kulalamikia ufisadi na gharama ya juu iliyotumiwa kuandaa kombe la dunia.
No comments:
Post a Comment