Mmiliki wa Manchester United mmarekani Malcom Glazer ameaga
dunia akiwa na umri wa miaka 85 .
Familia ya bwenyenye huyo ilinunua United kwa gharama ya Euro milioni 790
mnamo mwezi Mei mwaka wa 2005 licha ya pingamizi kali kutoka a kwa mashabiki wa
klabu hiyo.Wanawe mmarekani huyo waliozaliwa Marekani Byan, Joel, na Avram wote wamejumuishwa katika bodi ya klabu hiyo, huku Joel na Avram wakiwa wenyekiti wenza.
Kifo cha Glazer hakitarajiwi kuadhiri umiliki wa United, kwani familia hiyo bado inamiliki asilimia 90 za hisa za klabu hiyo .
Asilimia 10 inayosalia inamilikiwa na wenyehisa katika soko la hisa la NY stock Exchange.
United ambayo msimu uliopita ilitangaza faida kubwa ya asilimia 20 yaani pauni milioni 418 inakabiliwa na deni la zaidi ya pauni milioni 400.
Glazer aliyeugua kiharusi tangu mwaka wa 2006 amewaachia wanawe sita umiliki wa klabu hiyo ya Uingereza.
No comments:
Post a Comment