Na Mwandishi wangu
SERIKALI
kupitia Wizara ya Uchukuzi inayoongozwa na Dk. Harrison Mwakyembe inastahili,
pongezi kwa kupiga hatua kubwa kujenga na kuimarisha sekta ya usafirishaji wa
anga nchini.
Mkurugenzi
wa Msama Promotins Alex Msama, ametoa pongezi hizo siku chache baada ya Wizara
hiyo kuendelea kuonesha mafanikio makubwa katika utoaji wa huduma za anga
nchini.
Msama ambaye
pia ni mfanyabiashara maarufu amewahimiza Watanzania kujawa na uzalendo na
hivyo, kuliunga mkono Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) kwa kutumia huduma zake
zilizoboreshwa ili liweze kupambana na changamoto mbalimbali zilizopo katika sekta ya
usafirishaji wa anga nchini.
Alisema
hatua ya Wizara ya Uchukuzi kuwekeza katika usafiri wa anga inapaswa kuungwa
mkono na kila Mtanzania kwa maslahi ya taifa.
“Huduma
zinazotolewa na ATCL sasa ni nzuri na zenye ubora unaolingana na mazingira ya
sasa, hivyo ni vema sisi Watanzania tujivunie; kila Mtanzania anapaswa
kujivunia na kutumia huduma za shirika hilo.”
Hata hivyo,
alitoa rai kwa makampuni, taasisi zote za serikali na mtu mmoja mmoja kutumia
ndege ya shirika hilo linalofanya safari zake katika mikoa mbalimbali nchini.
Kwamba hatua pekee ya kuongeza ufanisi wa ATCL ni watu kutumia chao na kukilinda na kukituza.
Mpaka sasa
ATCL ina ndege mbili ikiwamo ya Jet 103, ambazo kwa muda mfupi, zimeonesha
ufanisi wa hali ya juu katika utoaji huduma wa safari za anga.
Aliongeza
kuwa amefurahishwa na huduma ya Ndege ya ATCL itokayo Dar kwenda Mwanza ambapo
alisema kuwa ndege hiyo ni nzuri na pia huduma zake ni nzuri na ikiwa angani
inatulia mpaka unajisahau kama upo ndani ya ndege.
Aidha
alisema kuwa ni vyema kila mtanzania akatumia ndege hii kwani kwa ndege zote
alizopanda kwenda Mwanza hii ni ndege bora zaidi.
Pia amewaasa
Watanzania kuwa wazalendo kama wenzetu wakenya ambao wamekuwa wazelendo kwa
kutumia ndege zao kila wafanyapo safari, na hivyo ni vema watanzania kutumia ndege za ATCL ili kusaidia shirika
hilo kutoka ndege mbili hadi kuongeza ndege zaidi.
No comments:
Post a Comment