Shule iliyokumbwa na kashfa
Mwalimu mkuu wa shule moja ya upili nchini Uingereza ameachishwa
kazi kufuatia utata kuhusu kanda ya ngono inayodaiwa kurekodiwa shuleni humo.
Mwenyekiti wa bodi ya shule alimwachisha kazi mwa muda mwalimu
mkuu Graham Daniels na mfanyakazi mwingine wa shule ambaye jina lake
halikutajwa baada ya malalamiko kutolewa kuwahusu wawili hao.
Taarifa
zinazohusiana
Kuachishwa kazi kwa mwalimu huyo kulitokea baada ya wanafunzi
kusambaza kanda hiyo kwa mitandao ya kijamii. Kanda hiyo ilikuwa na sauti za
watu wawili wakijihusisha na ngono katika chumba kimoja cha shule hiyo.
Hata hivyo wakuu wa bodi walisema kuwa shughuli za masomo
zinaendelea kama kawaida.
Mkuu wa bodi alisema: "shule imepokea malalamiko ambayo
hayakumtaja mtu yeyote lakini kufuatia madai hayo uchunguzi utafanywa.''
Mwalimu mkuu na mfanyakazi mwingine wa shule wameachishwa kazi
kutokana na madai hayo.
No comments:
Post a Comment